Matthew 24:3-8

3 aIsa alipokuwa ameketi kwenye Mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamjia faraghani, wakamuuliza, “Tuambie, mambo haya yatatukia lini, nayo dalili ya kuja kwako na ya mwisho wa dunia ni gani?”

4 bIsa akawajibu, “Jihadharini, mtu yeyote asiwadanganye. 5 cKwa maana wengi watakuja kwa Jina langu, wakidai, ‘Mimi ndiye Al-Masihi,’
Al-Masihi maana yake ni Masiya , yaani Aliyetiwa mafuta.
nao watawadanganya wengi.
6 eMtasikia habari za vita na matetesi ya vita. Angalieni msitishike, kwa maana haya hayana budi kutukia. Lakini ule mwisho bado. 7 fTaifa litainuka dhidi ya taifa, na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali. 8Haya yote yatakuwa ndio mwanzo wa utungu.

Copyright information for SwhKC